Baada ya mvutano mkubwa sasa Filamu ya maisha ya Tupac Shakur ‘All Eyez On Me’ itatoka siku hii….



Baada ya mvutano wa haki za muziki na kazi za Tupac Shakur kuisha sasa ile filamu ya maisha ya  2 Pac All Eyez On Me imepata tarehe rasmi ya kutoka.
Filamu hii iliyoongezwa na Benny Boom na kuigizwa na staa Demetrius Shipp Jr kama 2 Pac itatoka kwenye siku ya kuzaliwa ya 2 Pac.
Angekuwa hai angekuwa anafikisha miaka 46 ifikapo June 16, 2017.
Jamal Woolard ameigiza kama The Notorious B.I.G,  Dominic L. Santana ameigiza kama Suge Knight.
Staa wa “The Walking Dead’s” Danai Gurira ameigiza kama mama yake 2 Pac na Lauren Cohan ameigiza kama meneja Leila Steinberg.



<iframe width="480" height="270" src="https://www.youtube.com/embed/lQ0Tj2NgtaE" frameborder="0" allowFullScreen=""></iframe>

Hakuna maoni