TUZO ZA NNJE HAZINIPI SHIDA-JOH MAKINI

 Image result for joh makini



Msanii wa muziki wa hip hop kutoka Weusi, Joh Makini amewataka mashabiki wa muziki wa hip hop kuendelea kusubiria mambo mabubwa kutoka kwa wasanii wao huku akidai wasanii wa hip hop kutokuwa nominees kwenye tuzo za nje haimaanishi kwamba hawafanyi vitu bora.




           Akizungumza siku chace zilizopita alisema, Joh Makini amedai wasanii wa hip hop muda wao bado lakini wanafanya kazi nzuri ambazo zinapendwa mpaka nje ya mipaka.

            “Mimi suala la kutokuwa nominees kwenye tuzo za nje nalichukulia kawaida tu,” alisema Joh. “Kwasababu kutokuwa nominees au kuwa nominees haijalishi kwamba wewe huwezi kufanya kitu unachokifanya kwa ubora,” alisema Joh Makini.
Pia rapper huyo amesema mwaka 2016 ulikuwa mzuri kwake kutokana na kufanya kazi nyingi ambazo zimefanya vizuri kitaifa na kimataifa.

Hakuna maoni