DESIGNEER AINGIA KWENYE DENI KUBWA

Desiigner rapa wa G.O.O.D Music ya Kanye West anadaiwa zaidi ya bilioni moja za kibongo na kampuni ya kukodisha magari ya kifahari nchini Marekani.
Desiigner alikuwa akiendesha Ferrari ya mwaka 2014 na alipata nalo ajali June mwaka huu. Gari hio ilikodishwa na marafiki wawili wa Desiigner ambao pia wametajwa kutakiwa kulipa pesa kwneye deni hili.
Gari hio inathamani ya dola laki mbili na elfu ishirini $220k, ila kampuni hio inasema inataka kulipwa dola $500k ambazo nikama 1,089,900,000.00 za Tz kutokana na gari huo kutolewa sokoni na hio ni kama hasara waliyopata sababu halikutumika tena baada ya kugongwa.
Timu ya Desiigner inasema hii ni mara ya kwanza wanapata taarifa hizi….
feraree

Hakuna maoni