BURUDANI: ''DIAMOND NDIYE MSANII ANAYEKUBALIKA NAMIBIA'', CHIKUNE


13256693_640787786069078_1704542408_n 
Mshindi wa tuzo ya Afrimma 2016 kwenye kipengele cha Best Female, Southern Africa, Chikune kutoka Namibia amefunguka kwa kumtaja msanii wa Bongo Fleva anayekubalika zaidi nchini humo na sababu ya wasanii wa nchi hiyo kutofanya vizuri kwenye tuzo kubwa za Afrika.

Muimbaji huyo amesema, “Diamond anakubalika zaidi kwa sababu ni mburudishaji, mfanyabiashara na amefanikiwa kuwafanya mashabiki kufurahia muziki wake bila ya kujali lugha anayoitumia.”
Akiongea kuhusu kutofanya vizuri kwa wasanii wa nchi hiyo kwenye tuzo kubwa za Afrika, amesema, “Namibia ni kama bwawa la vipaji vya muziki, ila kuna mapungufu yanayotokana kwenye soko la muziki la ndani lililofunikwa na kivuli cha soko la muziki la Afrika Kusini.”
Kwa sasa muimbaji huyo anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Kapana’ aliouachia mwezi April mwaka huu.


Hakuna maoni